"Karibuni sana katika huduma ya kiroho ya Nuru Duniani FM-TV. Sisi ni kituo kinachotoa mafundisho ya neno la Mungu pamoja na maombi ya kurejesha imani kwa watu wote ulimwenguni. Huduma yetu iko Kisongo, Arusha, karibu na kiwanda cha A to Z Tanzania. Ili kufika panda magari ya kwenda Kisongo kiwandani, ukifika hapo uliza kwa mtumishi wa Mungu Paschal Thomas Makemba na utafika moja kwa moja. Ibadah yetu inaanza saa tatu kamili asubuhi hadi saa saba mchana kila Jumanne na Jumamosi. Mungu awabariki sana nyote mnaojiunga nasi kusikiliza injili ya kweli. Tunawakaribisha wote kusikiliza neno la uzima kila siku ili tujengane katika imani na upendo wa Kristo Yesu. Lengo letu ni kueneza habari njema za wokovu kwa kila kiumbe na kuleta matumaini pale ambapo hapana matumaini. Ungana nasi sasa kupokea